MigogoroSyria
Watu 16 wauawa katika shambulizi la anga mjini Aleppo
30 Novemba 2024Matangazo
Shirika hilo la Haki za Binaadamu la nchini Syria limesema shambulizi hilo lilipiga eneo la mji wa Aleppo ambao tayari unadhibitiwa na waasi.
Mapema, jeshi la Syria lilisema makumi ya wanajeshi wake wameuawa kaskazini mwa mji huo wa Aleppo na kuwafanya kurudi nyuma, hii ikiwa ni changamoto kubwa kwa Rais Bashar al Assad baada ya miaka mingi.
Jeshi hilo lakini limesema linajiandaa kwa mashambulizi ya kushtukiza ili kuirejesha mamlaka.