Watu 16 wauawa katika shambulizi la Israel, Gaza City
17 Septemba 2025
Matangazo
Maafisa hao pia wamesema zaidi ya nusu ya waathiriwa, waliuawa katika mashambulizi dhidi ya Gaza City, akiwemo mtoto na mama yake waliokuwa nyumbani mwao katika kambi ya wakimbizi ya Shati.
Katikati mwa Gaza, hospitali ya Al-Awda imesema kuwa shambulizi la Israel lililenga nyumba moja katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat na kuwauwa watu watatu ikiwa ni pamoja na mwanamke mjamzito.
Hata hivyo jeshi la Israel halikujibu mara moja ombi la tamko kuhusu mashambulizi hayo.
Wakati huo, muungano wa mashirika makubwa ya misaada, leo umeihimiza jumuiya ya kimataifa
kuchukua hatua kali kukomesha mashambulizi ya Israel Gaza City, baada ya tume ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kugundua kuwa Israel inafanya mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza.