1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNigeria

Watu 16 wauwawa kwenye shambulio jimbo la Plateau, Nigeria

25 Desemba 2023

Watu 16 wameuwawa kwenye shambulio lililotokea eneo la kaskazini kati mwa Nigeria, linalokumbwa kila wakati na mapigano baina ya jamii za wakulima na wafugaji.

Njia ya kuingia Jos, mji mkuu wa jimbo la Plateau, Nigeria
Jimbo la Plateau limekuwa kitovu cha mapigano kati ya jamii za wakulima na wafugaji nchini Nigeria.Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Hayo ni kulingana na jeshi la Nigeria ambalo limearifu kuwa mkasa huo umetokea katika kijiji cha Mushu kinachopatikana kwenye jimbo la Plateau.

Mkaazi mmoja wa kijiji hicho ameliambia Shirika la Habari la AFP kwamba walikuwa wamelala usiku wa manane kuamkia Jumapili, ndipo waliposikia milio ya risasi. Washambuliaji waliwauwa na kuwajeruhi baadhi ya wanakijiji na kuwateka nyara wengine.

Jimbo la Plateau linapatikana kwenye mpaka unaotenganisha eneo la kaskazini mwa Nigeria lenye idadi kubwa ya waislamu na kusini kwenye wakristo wengi na kwa miaka kadhaa sasa limekuwa kitovu cha mivutano ya kikabila na kidini.

Wengi ya jamii ya wafugaji ni waislamu na wakulima ni wakristo na mara kadhaa pande hizo mbili zimetumbukia kwenye mapigano yenye kuhusisha magenge ya watu wenye silaha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW