1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiKorea Kusini

Watu 167 waangamia katika ajali ya ndege Korea Kusini

29 Desemba 2024

Waokoaji wanahofia huenda watu wote 181 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameangamia isipokuwa watu wawili ambao wamenusurika.

Ajali ya ndege nchini Korea Kusini
Kulingana na taarifa iliyotolewa na maafisa wa kupambana na moto kwa familia za watu waliokuwemo ndani ya ndege, nafasi ya abiria waliokuwemo ndani kunusurika ni ndogo.Picha: Yonhap via REUTERS

Ndege ya abiria ya shirika la Jeju Air iliyowabeba abiria 181 kutoka Thailand kuelekea Korea Kusini, imeanguka usiku wa kuamkia leo ilipokuwa ikitua na kuwaka moto. Watu 167 wamethibitishwa kufariki kwenye ajali hiyo.

Waokoaji wanahofia huenda watu wote waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameangamia isipokuwa watu wawili ambao wamenusurika.

Chanzo kamili cha ajali hiyo hakijabainika lakini maafisa wametaja hali mbaya ya hewa na ndege kuingia kwenye injini kuwa huenda zikawa sababu.

Video ilisoyambazwa mitandaoni ilionyesha ndege hiyo ikitua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Muan Korea Kusini, kisha ikapoteza mwelekeo huku injini zake zikifuka moshi kabla ya kugonga ukuta, kulipuka na kuwaka moto.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na maafisa wa kupambana na moto kwa familia za watu waliokuwemo ndani ya ndege, nafasi ya abiria waliokuwemo ndani kunusurika ni ndogo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW