Watu 17 wauawa katika shambulizi la kutokea angani Khartoum
17 Juni 2023Shambulizi hilo ni moja ya mashambulizi makubwa kabisa katika mapigano yanayoendelea kwenye maeneo ya Khartoum na miji mingine nchini Sudan kati ya majenerali wawili wanaozozania madaraka.
Soma pia: Watoto milioni 1 wameachwa bila makao katika mapigano Sudan
Haikuwa wazi iwapo shambulizi hilo lilifanywa na ndege ama droni. Kulingana na wizara ya afya, shambulizi hilo lilitokea katika eneo la Yormouk, kusini mwa Khartoum ambako kunashuhudiwa mapigano makali katika wiki za karibuni na karibu nyumba 25 ziliharibiwa.
Majeruhi wamelazwa hospitali kwa matibabu zaidi. Taarifa ya kikosi cha Dharura cha RSF kinachopambana na serikali imesema ndege ya jeshi ilishambulia eneo hilo na kuwaua raia na kuongeza kuwa iliifanikiwa kuidungua ndege ya kivita chapa MiG.