1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Watu 17 wauawa katika ufyatulianaji risasi Afrika Kusini

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

Watu kumi na saba wakiwemo wanawake 15 wameuawa katika ufyatulianaji wa risasi wakati wa mauaji yaliyotokea katika matukio mawili tofauti nchini Afrika Kusini.

Polisi imesema mauaji hayo yalikitokea usiku wa kuamkia Jumamosi katika mji wa Lusikisiki, jimbo la Western Cape
Polisi imesema mauaji hayo yalikitokea usiku wa kuamkia Jumamosi katika mji wa Lusikisiki, jimbo la Western Cape Picha: Rogan Ward/REUTERS

Brigedia Athlenda Mathe, msemaji wa polisi ya Afrika Kusini amesema msako unaendelea kuwatafuta washukiwa hao.

Taarifa ya polisi imesema wanawake kumi na wawili na mwanaume mmoja waliuawa katika nyumba moja na wanawake watatu na mwanamume mwengine waliuawa katika nyumba nyingine. Muathiriwa mwengine mmoja amelazwa hospitalini akiwa kati hali mbaya.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani. Na visa vya mauaji ya watu wengi vimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Huku wakati mwingine watu hulengwa wakiwa nyumbani mwao.