1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 18 wafa katika ajali ya ndege huko Kathmandu

Josephat Charo
24 Julai 2024

Msemaji wa jeshi la polisi la Nepal Dan Bahadur Karki amesema ndege ya shirika la Saurya Airlines ilikuwa imewabeba maafisa wawili wa ndege hiyo na wafanyakazi 17 wa kampuni hiyo.

Nepal Kathmandu | Ajali ya ndege
Mabaki ya ndege iliyopata ajali NepalPicha: Sujan Gurung/AP/picture alliance

Watu 18 wamekufa baada ya ndege ya abiria kuanguka muda mfupi baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Kathmandu, nchini Nepal.

Polisi katika mji mkuu Kathmandu wamesema rubani wa ndege hiyo ameokolewa kutoka kwa mabaki. Msemaji wa jeshi la polisi la Nepal Dan Bahadur Karki amesema ndege ya shirika la Saurya Airlines ilikuwa imewabeba maafisa wawili wa ndege hiyo na wafanyakazi 17 wa kampuni hiyo.

Mkasa wa tetemeko la ardhi: Tetemeko la ardhi nchini Nepal lauwa watu 138

Karki aidha amesema rubani wa ndege hiyo anaendelea kutibiwa hospitali akiwa hali mahututi na miili 18 tayari imeopolewa, ukiwemo mmoja wa raia wa kigeni. Amesema wanaendelea na mchakato wa kuipela miili hiyo katika chumba cha kuhifadhia maiti. Mamlaka ya usafiri wa anga ya Nepal imesema raia wa kigeni aliyekufa ni raia wa Yemen.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW