18 wafariki dunia katika kambi ya wakimbizi huko Cameroon
4 Agosti 2020Shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi(UNHCR) limepeleka kikosi cha dharura kaskazini mwa Cameroon baada ya watu takribani 18 waliohamishwa kuuwawa katika shambulio la mlipuko wakati wakihama kutoka katika kambi ya wakimbizi, msemaji wa shirika hilo amesema Jumanne.
Kikundi cha kigaidi cha Kiislam cha Boko Haram kinashukiwa kuwa nyuma ya shambulio hilo lililotokea mapema majira ya usiku wa Jumapili, msemaji wa UNHCR Babar Baloch, amesema katika mkutano na wandishi wa habari kutoka Geneva.
Watu wengine 11 walijeruhiwa katika tukio hilo karibu na Nguetchewe, kijiji kilicho karibu na mpaka wa Nigeria.
Baloch alisema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya vurugu za Boko Haram na vikundi vingine vyenye silaha huko katika mikoa ya kaskazini mnamo mwezi Julai.
Mkoa huo uliopo kati ya Nigeria na Chad unahifadhi baadhi ya wakimbizi 322,000 wa ndani wa Cameroon pamoja na wakimbizi wa Wanigeria 115,000.
Kameroon imeshuhudia mashambulio ya Boko Haram 87 kwenye mpaka wake wa kaskazini na Nigeria hadi sasa mwaka huu.
"Tukio hilo pia ni ukumbusho wa kusikitisha wa ukali wa ukatili wa vurugu katika eneo kubwa la bonde la ziwa Chad," Baloch alisema akiashiria watu milioni 3 ambao wamelazimika kukimbia ndani kaskazini mashariki mwa Nigeria, Kameroon Chad na Niger.
Makumi kwa maelfu wamekufa mikononi mwa washirika wa Sunni tangu mwaka 2009.