1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia shule Gaza na kuuwa wafanyakazi wa UN

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Watu 18 wameuwawa baada ya jeshi la Israel kulipua shule kwenye eneo la Nuseirat, Gaza. Kulingana na shirika la ulinzi wa raia katika ukanda huo limesema , miongoni mwa waliouwawa ni wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Ukanda wa Gaza | Shambulio la shule.
Watu wakiwa wametawanyika nje ya shule ambayo inatumiwa kujihifadhi Wapalestina waliokimbia mapigano, baada ya Israel kushambulia.Picha: Eyad Baba/AFP/Getty Images

Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal  amewataja wengine waliouwawa kuwa ni watoto pamoja na wanawake. Watu wengine 18 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Soma pia:Vikosi vya Israel vyaendelea kuushambulia Ukanda wa Gaza

Hayo yanajiri wakati Wizara ya Afya chini ya kundi la Hamas kwenye ukanda huo ikiarifu kuwa hadi sasa zaidi ya watu 41,100 wameuwawa tangu vita kati ya Israel na kundi la Hamas vilipoanza mwezi Oktoba mwaka jana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW