MigogoroSudan Kusini
Watu 18 wauawa Sudan Kusini kufuatia mzozo wa ardhi
7 Februari 2024Matangazo
Hayo ni kulingana na Gavana wa muda wa jimbo hilo Arkenjelo Anyar ambaye amesema kuwa baadhi ya watu waliuliwa kwa kuchomwa moto.
Majambazi hao kutoka jimbo jirani la Warrap waliteketeza kwa moto eneo la soko, makazi ya raia pamoja na kituo cha polisi huko Tharkueng Payam kufuatia mzozo wa ardhi. Wanawake, watoto na wazee ni miongoni mwa waliouawa huku watu wengine zaidi ya 2,000 wakilazimika kuyahama makazi yao.
Jumatano iliyopita, watu 39 waliuawa na makumi ya wengine walijeruhiwa kufuatia ghasia zilizozuka kati ya makundi hasimu ya wafugaji katika majimbo ya Warrap na yale yaliopo katikati mwa nchi hiyo. Sudan Kusini ni moja ya nchi masikini zaidi duniani licha ya kuwa na rasilimali ya mafuta.