JamiiBurkina Faso
Watu 19 wauawa Burkina Faso kwenye shambulizi la wanamgambo
13 Februari 2023Matangazo
Afisa mmoja wa ngazi ya juu ameliambia shirika la habari la AFP kwamba miongoni mwao ni watu saba ambao ni wanchama wa kikosi cha wasamaria wema VDP waliouawa Alhamisi usiku wakati Kijiji cha Dembo kilichoko kaskazini magharibi mwa nchi kiliposhambuliwa.
Hapo jana, kundi linalodaiwa kuwa la kigaidi liliwaua watu 12 wakiwemo wanachama wawili wa VDP katika Kijiji cha Yargatenga, kilichoko mashariki, mpaka wan chi hiyo ya Togo na Ghana. Hayo ni kulingana na duru katika eneo hilo.