1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Nigeria: Watu 2 wafariki kufuatia mlipuko Ubalozi wa Canada

8 Novemba 2023

Watu wawili wamekufa na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya kutokea mlipuko katika Ubalozi wa Canada mjini Abuja nchini Nigeria. Kufuatia tukio hilo, Ubalozi huo umetangaza kusitisha shughuli zake kwa muda.

Askari jeshi na polisi wakiwa katika tukio la mlipuko Abuja, Nijeria
Askari jeshi na polisi wakiwa katika tukio la mlipuko Abuja, NijeriaPicha: dapd

Idara ya serikali ya Canada inayohusika na mahusiano ya kimataifa, imesema uchunguzi unaendelea ili kufichua chanzo cha mlipuko huo lakini uchunguzi wa awali unaashiria ajali iliyotokea katika chumba cha jenereta badala ya kitendo cha makusudi.

Soma pia:Shambulizi la bomu laua watu 30 Nigeria

Rais wa Nigeria Bola Tinubu pamoja na Ubalozi huo wametoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia ahueni ya haraka wale wote waliojeruhiwa katika tukio hilo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW