1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Watu wawili wakamatwa kwa uchochezi Hong Kong

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Polisi mjini Hong Kong wamesema watu wawili wamekamatwa kwa uchochezi chini ya sheria mpya ya usalama wa taifa. Tuhuma zinazowakabili watu hao zinatajwa kuwa ni kusambaza chuki dhidi ya China na mamlaka zake za ndani.

Hongkong
Polisi wa Hong Kong wakimtia nguvuni mmoja wa waandamanaji wanaounga mkono demokrasia Juni 4, 2024 Picha: Tyrone Siu/REUTERS

Taarifa ya polisi imewataja watu hao waliokamatwa Ijumaa kuwa ni mwanamume mwenye miaka 41 na mwanamke mwenye miaka 28. Wametiwa nguvuni, siku moja baada ya kituo cha habari cha Stand News kinachounga mkono demokrasia na wahariri wawili wa zamani kukutwa na hatia ya uchochezi. Uamuzi huo ni wakwanza tangu Hong Kong ilipoingia chini ya utawala wa China mwaka 1997.

Soma zaidi: China yawakemea wanaokosoa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong

Wakosoaji wanadai kuwa, maafisa katika mji huo wamekuwa wakitumia sheria ya uchochezi kuwalenga wakosoaji wa serikali na kuwanyamazisha wapinzani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW