SiasaSierra Leone
Watu 20 waliuwawa shambulizi la Jumapili nchini Sierra Leone
28 Novemba 2023Matangazo
Hayo yameelezwa na maafisa wa serikali siku mbili baada ya taifa hilo la Afrika Magharibi kutikiswa na kile viongozi wake wamekitaja kuwa shambulizi lililoratibiwa na wanajeshi "wasaliti".
Msemaji wa jeshi la taifa, Kanali Issa Bangura, ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa miongoni mwa watu 20 waliouwawa wamo wanajeshi 13, wanamgambo 3 na afisa mmoja wa polisi.
Imearifiwa pia wafungwa 1,890 walitoroka kutoka jela ya Pademba baada ya washambuliaji kuivamia.
Hata hivyo hali ya kawaida imerejea kwenye mji mkuu Freetown na rais Julius Maada Bio alikwishatangaza kwamba karibu viongozi wote wa shambulio la Jumapili wamekamatwa.