Watu 20 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Misri
21 Novemba 2011Matangazo
Vikosi vya usalama vilitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi kuzuia waandamaniji waliotaka kudhibiti boma lililopo karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani. Mamia ya waandamanaji katika uwanja wa Tahrir wamekuwa wakiushinikiza utawala wa kijeshi nchini humo kuharakisha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia. Vurugu hizo zilianza pale ambapo polisi walipoyaondoa mahema ya kiasi ya waaandamanji 100 walioweka kambi katika uwanja huo baada ya maandamano ya ijumaa.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Hamidou, Ummilkheir