1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Watu 20 wauawa Baluchistan kuekelea uchaguzi wa Pakistan

7 Februari 2024

Watu zaidi ya 20 wameuawa baada ya miripuko miwili kutokea karibu na afisi za wanasiasa wawili wanaogombea nyadhifa katika uchaguzi wa Pakistan katika mkoa wa kusini magharibi wa Balochistan.

Wanajeshi wa Pakistan wakiwa karibu wa mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.
Wanajeshi wa Pakistan wakiwa karibu wa mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.Picha: Banaras Khan/AFP/Getty Images

Maafisa katika eneo hilo walisema miripuko hiyo imezua wasiwasi kuhusiana na usalama kuelekea uchaguzi wa Alhamis (Februari 8).

Pakistan inaingia katika uchaguzi wakati kukiwa na ongezeko la mashambulizi ya wanamgambo katika miezi ya hivi karibuni na kufungwa jela kwa Imran Khan aliyekuwa mshindi wa uchaguzi uliopita. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW