1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi lasababisha mauaji ya watu 20 Afghanistan

3 Novemba 2025

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika kipimo cha Richter limeitikisa Afghanistan usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu 20 huku wengine zaidi ya 300 wakijeruhiwa.

Afghanistan 2025 | Tetemeko la ardhi lasababisha maafa makubwa
Watu 20 wauwawa na wenggine kujeruhiwa katika tetemeko kubwa la ardhi Afghanistan Picha: Afghan Red Crescent/REUTERS

Shirika la Marekani la utafiti wa kijiolojia  limesema tetemeko hilo lilipiga eneo la Kusini Magharibi mwa mji wa Khulm.

Tetemeko hilo pia limepiga kina cha kilomita 28 ardhini na karibu na Mazar-e Sharif, mji ulio na karibu watu 523,000.

Shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga huko Afghanistan limesema litatoa baadae taarifa kuhusiana na vifo zaidi na hasara ya janga hilo.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha ukubwa wa hasara ya tetemeko hilo kwa wakati lilipotokea. Video za juhudi za kuwaokoa watu waliokuwa wamenasa chini ya vifusi zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.