JangaLibya
Watu 2,000 wahofiwa kufariki Libya kufuatia Kimbunga Daniel
12 Septemba 2023Matangazo
Mafuriko hayo yameshuhudiwa baada ya kimbunga Daniel kuipiga kanda ya Bahari ya Mediterrania. Taarifa hiyo ya vifo vya watu 2,000 imetolewa na Waziri Mkuu wa serikali ya Mashariki mwa Libya Ossama Hamad alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha al-Masar. Kiongozi huyo ameongeza pia kuwa kati ya watu 5,000 na 6,000 hadi sasa haijulikani waliko.
Mkurugenzi mmoja wa shirika la kimataifa la misaada ameiambia DW kwamba Libya inashuhudia maafa makubwa. Uharibifu mkubwa zaidi umeshuhudiwa katika jiji la Derna kwenye jimbo la Jabal al-Akhdar na katika viunga vya Al-Marj.
Vikosi vya uokoji vimepelekwa kwenye mji huo, ulioko takriban kilometa 900 mashariki mwa mji mkuu, Tripoli.