JangaAfrika
Watu 2,000 wapoteza maisha mjini Derna kufuatia mafuriko
12 Septemba 2023Matangazo
Mamlaka nchini humo imeeleza kuwa, inakadiriwa kuwa watu 2,000 wanaaminika kupoteza maisha katika mji wa Derna.
Kimbunga cha Daniel kimesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mengi ya mashariki mwa Libya, lakini uharibifu mkubwa umetokea katika mji wa Derna ambapo mvua na mafuriko yamevunja mabwawa na kusomba vijiji.
Soma pia:Kimbunga Daniel chaua watu zaidi ya 2,000 Libya
Waziri Mkuu wa serikali upande wa mashariki ya Libya Ossama Hamad amesema maelfu ya watu hawajulikani waliko na kwamba wengi wao wanaaminika kusombwa na maji.
Shirika la hilali nyekundu la Libya limesema leo kuwa, timu yao imehesabu zaidi ya watu 300 waliokufa mjini Derna. Serikali ya Mashariki mwa Libya imeutangaza mji huo wa Derna kama eneo la maafa.