1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu 21 wafariki ajali ya boti Ufiilipino

27 Julai 2023

Yapata watu 21 wamefariki dunia na wengine 40 kuokolewa baada ya boti moja ya abiria kupinduka na kuzama leo, iliposukumwa na upepo mkali katika Ziwa Laguna kusini mashariki mwa Mji Mkuu wa Ufilipino, Manila.

Flash-Galerie Tote nach Schiffsunglück in Moskau
Picha: picture alliance/dpa

Kulingana na polisi, operesheni ya uokoaji inaendelea ila haikutoa idadi kamili ya watu waliokuwa ndani ya boti hiyo ya MBCA Princess Aya, iliyozama katika mkoa wa Rizal.

Mkasa huo umetokea baada ya abiria kusogea ghafla katika upande mmoja wa boti hiyo kutokana na hofu, upepo mkali ulipovuma, muda mfupi baada ya kuanza safari yao.

Kulingana na walinzi wa pwani, boti hiyo inadaiwa kupinduka katika eneo la umbali wa mita 46 tu kutoka ufukweni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW