JangaDjibouti
Watu 21 wamekufa baada ya boti ya wahamiaji kuzama Djibouti
24 Aprili 2024Matangazo
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji - IOM limesema boti iliyokuwa na wahamiaji 77 wakiwemo watoto, ilizama katika pwani ya taifa hilo.
Msemaji wa IOM Yvonne Ndege amesema wanashirikiana na maafisa wa Djibouti katika juhudi za uokoaji.
Aprili 8, Boti nyingine iliyokuwa na zaidi ya watu 60 ilizama katika pwani ya Godoria. Takriban wiki mbili zilizopita, boti nyingine iliyowabeba wahamiaji, wengi wao wakiwa raia wa Waethiopia ilizama katika pwani ya Djibouti na kusababisha vifo vya watu kadhaa.