1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 21 wauwawa Somalia

22 Aprili 2023

Jeshi nchini Somalia leo hii limefanikiwa kulidhibiti shambulizi la wapiganaji wenye itikadi kali katika maeneo ya mbali ya taifa hilo na kuwaua wanamgambo 18 wa al-Shabab

Somalia Bombenanschlag in Mogadishu
Picha: Farah Abdi Warsameh/AP Photo/picture alliance

Jeshi nchini Somalia leo hii limefanikiwa kulidhibiti shambulizi la wapiganaji wenye itikadi kali katika maeneo ya mbali ya taifa hilo na kuwaua wanamgambo 18 wa al-Shabab.Afisa wa juu wa jeshi, Jenerali Mohamed Ahmed Taredisho amesema takribani raia watatu ambao wanaelezwa kuwa ni wazee wa kimila wamekufa katika mapigano hayo yalitokea karibu na mji wa Masagaway. Masagaway iko katika mkoa wa kati wa Galgadud na kuna kambi kijeshi. Mkazi mmoja katika eneio hilo, Yusuf Sheikh aliliambia Shirika la Habari la Associated Press kuwa wanamgambo walivamia kambi hiyo, wakachukua silaha na kuchoma moto magari ya kijeshi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW