1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaBrazil

Watu 22 wapoteza maisha ajali ya basi nchini Brazil

21 Desemba 2024

Watu wasipungua 22 wamekufa leo Jumamosi baada ya basi la abiria kupinduka na kushika moto kwenye jimbo la kusini mashariki mwa Brazil la Minas Gerais.

Picha ya eneo la mkasa wa basi la abiria nchini Brazil
Picha ya eneo la mkasa wa basi la abiria nchini Brazil.Picha: Belo Horizonte Military Fire Department/Handout/REUTERS

Maafisa wa jimbo hilo wamesema ajali hiyo ilitokea pale basi hilo la abiria lilipopasuka tairi na kupoteza mwelekeo na kisha kugongana na lori la mizigo mnamo majira ya asubuhi kwa saa za Brazil.  Inaarifiwa chombo hicho kilikuwa kimewabeba abiria 45 kilipoondoka mji wa Sao Paulo mnamo alfajiri.

Taarifa ya idara ya zimamoto wa jimbo la Minas Gerais wamesema baada ya jitihada ya saa kadhaa walifanikiwa kuuzima moto na kuipata miili ya watu 22 waliokwama ndani ya basi na kutetekea. Idara hiyo pia imesema watu wengine 13 wamejeruhiwa na wamepelekwa kwenye hospitali ya mji jirani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW