1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu 22 wauwawa shambulizi la anga Sudan

8 Julai 2023

Watu wasiopungua 22 wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi la anga lililofanywa na Jeshi la Sudan magharibi mwa mji wa Omdurman.

FILE PHOTO: Sudan's Khartoum running low on food and medicine as fighting rages
Picha: El-Tayeb Siddig/REUTERS

Hayo yameelezwa na wizara ya afya ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Hakuna maelezo yoyote ya ziada yaliyotolewa kuhusu shambulizi hilo lakini jeshi la nchi hiyo lilisema kuptiia ukurasa wake wa Facebook kwamba vikosi vyake vimewauwa askari 20 walioasi na kuharibu silaha zao.

Katika wiki za karibuni mapigano yameongezka kwenye  mji wa Omrduman kati ya jeshi la Sudan na Kikosi kilichoasi cha wapiganaji wa akiba, RSF.

Sudan imetumbukia kwenye mzozo tangu April 15 pale mapigano yalipozuka kati ya pande mbili zinazowatii majenerali wawili wanaowania madaraka. Hadi sasa juhudi za kusitisha mapigano hayo  zimekwama.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW