Watu 23 wauwawa Maiduguri nchini Nigeria
17 Machi 2026
Matangazo
Watu wasiopunguwa 23 wameuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mashambulizi yanayodhaniwa kuwa ya kujitowa muhanga yaliyofanywa usiku wa kuamkia leo katika mji wa Maiduguri, Kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mashambulio hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika mji huo ndani ya kipindi cha hivi karibuni.
Wakaazi na watowa huduma ya dharura wameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba miripuko iliripotiwa katika maeneo matatu yaliyokuwa na msongamano wa watu kwenye mji mkuu huo wa jimbo la Borno ikiwa ni pamoja na kwenye soko kuu na eneo la kuingia hospitali ya mafunzo ya chuo kikuu cha Maiduguri.
Hakuna kundi limedai kuhusika na mashambulio hayo japo yanashukiwa kufanya na Boko Haram.