1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu 24 wauwawa katika shambulio la bomu, Pakistan

9 Novemba 2024

Polisi nchini Pakistan wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu 24 wameuwawa, huku zaidi ya 40 wakijeruhiwa katika shambulio la bomu katika kituo cha treni mjini Quetta Kusini Magharibi mwa Pakistan.

Pakistan Quetta 2024 | Bomu katika kituo cha treni
Watu 24 wameuwawa katika shambulio la bomu kwenye kituo cha treni, PakistanPicha: Arshad Butt/AP Photo/picture alliance

Inspekta jenerali wa polisi wa Balochistan, Mouzzam Jah Ansari, amethibitsiaha mauaji ya watu hao 24,  huku akisema walengwa walikuwa wanajeshi wa taasisi moja ya kijeshi iliyoko karibu. Mouzzam amesema waliojeruhiwa wako katika hali mbaya. Mohammed Hammad mmoja ya walioshuhudia tukio hilo amesema miili ya watu imetapakaa kote katika kituo hicho.

“Watu walikuwa wakikimbia huku na kule wakiwa na mshituko mkubwa, baadhi wamejeruhiwa, wengine walikuwa hawana miguu, mikono ya wengine pia ilikuwa imeripuliwa , watu walikuwa tu wanakimbia huku na kule," alisema Hammad.

Waziri Mkuu Shehbaz Sharif amelilaani tukio hilo akisema waliohusika watawajibishwa.

Watu wanane wauawa katika shambulizi Pakistan

Jeshi la ukombozi la he Baloch ambalo ni kundi la wanamgambo wanaotakakujitenga wamekiri kuhusika na shambulizi hilo katika taarifa waliyoituma kwa shirika la Reuters. Jeshi hilo linataka uhuru wa Balochistan, mkoa ulio na idadi ya watu milioni 15 unaopakana na Afghanistan upande wa kaskazini na Iran upande wa magharibi.  

Wanamgambo hao ni moja ya makundi mengi ya wanamgambo nchini Pakistan wanaopigana na serikali yakiishutumu kutumia vibaya rasilimali za mkoa huo uliotajiri kwa gesi na madini mengine. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW