1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Watu 24 wauawa Ukraine katika wimbi jipya la mashambulizi

Saleh Mwanamilongo
29 Desemba 2023

Mamlaka nchini Ukraine imesema Urusi ilirusha makombora 122 na makumi ya ndege zisizo na rubani katika mji mkuu wa Kiev na maeneo maeneo manegine ya nchi hiyo.

Watu 24 wauliwa na wengine 133 kujeruhiwa katika wimbi la mashambulizi ya Urusi nchini Urakine
Watu 24 wauliwa na wengine 133 kujeruhiwa katika wimbi la mashambulizi ya Urusi nchini UrakinePicha: Nina Liashonok/Avalon/Photoshot/picture alliance

Valerii Zuluzhnyi, mkuu wa jeshi la Ukraine amesema kikosi cha anga cha Ukraine kimedungua idadi kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani aina ya Shahed usiku kucha. Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Wanahewa la Ukraine Mykola Oleshchuk aliandika kwenye mtandao wake wa Telegraph kwamba lilikuwa shambulio kubwa zaidi la anga tangu uvamizi wa Urusi mnamo Februari 2022. Kulingana na jeshi la anga la Ukraine, shambulio kubwa zaidi la hapo awali lilikuwa Novemba 2022 wakati Urusi iliporusha makombora 96 ​​dhidi ya Ukraine.

Takriban watu 130 walijeruhiwa na idadi isiyojulikana kuzikwa chini ya vifusi wakati wa shambulio. Miongoni mwa majengo yaliyoripotiwa kuharibiwa kote Ukraine walikuwa hospitali ya uzazi, vitalu na shule. Huko Boyarka, mji ulio karibu na Kyiv, vifusi vya ndege isiyo na rubani vilianguka juu ya nyumba na kuwasha moto.

''Vifusi vinaendelea kubomolewa''

Andrii Korobka mkaazi wa Boyarka alisema mamake alikuwa amelala karibu na chumba hicho ambapo mabaki hayo yalitua na kupelekwa hospitalini kutokana na mshtuko. Oleh Kiper, gavana wa jimbo la Odesa amesema hali ni mbaya katika jimbo hilo.

"Leo, tulirekodi waathiriwa 17. Watu watatu waliothibitishwa wamekufa hii ni matokeo ya awali. Vifusi vinaendelea kubomolewa, na katika maeneo mengine, moto bado haujadhibitiwa. Wachunguzi wote na vikundi vya watendaji, raia wanaohusika, na huduma zingine zinahusika kusaidia watu kadri inavyowezekana. Katika eneo hilo, msaada unaohitajika wa kisaikolojia hutolewa kwa waathiriwa wote.'', alisema  Kiper.

Umoja wa mataifa walaani mashambulizi ya Urusi

Ukraine yaziarai nchi za magharibi kuendelea kuipa misaada Picha: DW

Mkuu wa Tume ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amelaani wimbi la mashambulizi ya Urusi kote Ukraine na kuitaka Moscow kusitisha mashambulizi mara moja.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy asema vikosi vya Urusi vlitumia aina mbalimbali za silaha, ikiwa ni pamoja na makomba ya masafa marefu. Msemaji wa jeshi la anga la Ukraine Yurii Ihnat amesema mashambulizi ya leo yamehusisha aina zote za makombora, ikiwemo makombora ya kisasa ya Kinzhal, makombora ya masafa marefu chapa S-300, pamoja na droni za masafa marefu zilizotengenezwa nchini Iran.

Mashambulizi hayo yaliodumu kwa takribani saa 18 yalioanza Alhamisi na kuendelea usiku kucha, yamekuja siku chache baada ya Ukraine kuishambulia meli ya kivita ya Urusi katika bandari ya Feodosia katika rasi ya Crimea, katika pigo kubwa kwa jeshi la majini la Urusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba asema ukubwa wa shambulio hilo unapaswa kuamsha watu wote juu ya kuendelea kuisaidia Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW