SiasaUrusi
Watu 25 wauawa katika shambulio la makombora mjini Donetsk
22 Januari 2024Matangazo
Kiongozi anayeungwa mkono na Urusi katika mji wa Donetsk Denis Pushilin, amesema kuwa watu wengine 20 wakiwemo watoto wadogo wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Ameongeza kuwa, askari wa Ukraine ndio waliofanya shambulio katika soko hilo lenye shughuli nyingi. Jeshi la Ukraine hata hivyo halijatoa kauli yoyote juu ya shambulio hilo.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Ukraine vimeonyesha picha na vidio za soko lililoharibiwa vibaya.
Meya wa mji wa Donetsk Alexey Kulemzin amelaani shambulio hilo na kuliita la "kinyama" lililofanywa na askari wa Ukraine.