1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 25 wauawa kwenye mapigano nchini Pakistan

Josephat Charo
26 Septemba 2024

Watu wapatao 25 wameuliwa kufuatia siku kadhaa za makabiliano makali kati ya waumini Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni waliojihami na silaha kuhusiana na mgogoro wa ardhi kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Mlipuko wa bomu katika Msikiti wa Kishia Pakistan 2022
Mlipuko wa bomu katika Msikiti wa Kishia Pakistan 2022Picha: Muhammad Sajjad/AP/picture alliance

Watu wapatao 25 wameuliwa kufuatia siku kadhaa za makabiliano makali kati ya waumini Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni waliojihami na silaha kuhusiana na mgogoro wa ardhi kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Mapiganohayo yaliyoanza mwishoni mwa juma lililopita katika wilaya ya Kurram, mkoa wa kaskazini magharibi wa Khyber Pakhtunkhwa unaopakana na Afghanistan, yaliendelea jana Jumatano.

Maafisa wanasema watu kadhaa kutoka pande zote mbili wamejeruhiwa tangu Jumamosi iliyopita. Msemaji wa serikali ya jimbo Barrister Saif Ali, amesema mamlaka wakisaidiwa na wazee wa makabila wanajaribu kutuliza hali ya wasiwasi na pande zote zimekubali kufanya mazungumzo ya amani kufuatia mazungumzo yaliyofanyika Kurram.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW