28 waangamia baada ya kituo cha mafuta kushambuliwa Sudan
8 Desemba 2024Matangazo
Mtandao huo pia umetahadharisha kwamba idadi ya waliojeruhiwa huenda ikazidi kupanda.
Jeshi la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan ambalo limekuwa likipambana na wapiganaji wa wanamgambo la RSF wanaoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo tangu mwezi Aprili wamekuwa wakisonga mbele kuingia mjini humo katika wiki za hivi karibuni kwa lengo la kuudhibiti mji huo.
Mashambulio ya RSF yauwa watu wawili katika kambi ya wakimbizi Darfur
Tangu kuanza kwa machafuko ya Sudan, maelfu ya watu wameuawa huku raia milioni 11 wakipoteza makaazi yao na kusababisha moja ya mgogoro mbaya zaidi wa kibinaadamu kuwahi kushuhudiwa duniani. Hiyo ni kulingana na Umoja wa Mataifa.