1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 28 wameuwawa katika shambulio lililofanywa na Ukraine

Hawa Bihoga
4 Februari 2024

Urusi imesema idadi ya watu waliouawa kwenye duka la kuoka mikate mjini Lysychansk, imeongezeka na kufikia watu 28. Watu hao waliuawa katika mashambulizi ya majeshi ya Ukraine na miongoni mwao ni mtoto mmoja.

Lysychansk, Ukraine | Mabaki ya duka la kuoka mikate baada ya kushambuliwa
Duka la kuoka mikate lililoshambuliwa na majeshi ya UkrainePicha: Russian Emergency Ministry Press Service/AP/picture alliance

Wizara ya hali ya dharura ya Urusi kupitia mtandao wa Telegram imesema kuwa jiihada za uokozi bado zinaendelea katika duka hilo maarufu, na tayari watu wapatao kumi wameokolewa.

Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi imesema, silaha zilizotumika katika kutekeleza mashambulizi hayo ni zile ambazo Ukraine ilipokea kama msaada wa kijeshikutoka kwa washirika wake nchi za Magharibi na kuongeza kuwa inatarajia mashirika ya kimataifa kukemea haraka vitendo hivyo.

Soma pia:Urusi yailaumu Marekani kwa kuchochea vita vyake na Ukraine

Katika miezi ya hivi karibuni vikosi vya Ukraine vimeonekana kusionga mbele kwenye uwanja wa vita, lakini mapigano yameendelea kuwa makali kwa pande zote mbili msimu huu wa baridi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW