1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 286 wamejeruhiwa katika maandamano Morocco

1 Oktoba 2025

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imesema maafisa 263 wa vikosi vyake vya usalama na raia 23 wamejeruhiwa katika maandamano yaliyogeuka kuwa ghasia kwenye miji mingi ya nchi hiyo Jumanne usiku.

Rabat, Morocco 2025 | Polisi wakiwa na waandamanaji
Maandamano hayo yanapinga kushindwa kwa utawala kushughulikia masuala muhimu ya maishaPicha: Abdel Majid Bziouat/AFP/Getty Images

Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa Jumatano imeeleza kuwa waandamanaji walitumia visu na kurusha vilipuzi na mawe.

Waandamanaji wa Morocco wanataka mageuzi katika sekta ya afya na elimu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu 409 wamekamatwa na polisi wakihusishwa na ghasia hizo.

Katika mji wa Casablanca, waandamanaji 24 walioweka vizuizi kwenye barabara kuu wanachunguzwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW