Watu 30 wakamatwa kwa magendo ya binaadamu Uingereza
23 Septemba 2024Serikali ya Uingereza imesema vikosi vya usalama vya ndani na vya kimataifa vimefanya msako kwenye miji ya Belfast, Liverpool, Luton na Scotland ikiwa sehemu ya operesheni yao ya siku tatu.
Operesheni hiyo ilijumuisha upekuzi kwenye bandari kuu, viwanja vya ndege na barabara kuu.
Zaidi ya paundi 400,000 fedha taslimu na nyaraka kumi za kughushi zimekamatwa kwenye msako huo.
Soma zaidi: Uingereza kutumia fedha za mpango tata wa wahamiaji kwa ajili ya kuimarisha usalama
Waziri mwenye dhamana ya mipaka na wakimbizi, Angela Eagle, amesema serikali yake haitayaachia magenge ya wahalifu kuwanyonya watu na kuhatarisha maisha yao kwa tamaa za fedha.
Uingereza inakabiliwa na wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia kwenye kisiwa kikuu cha England kwa nia ya bahari.