1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 30 wauawa katika mashambulizi ya waasi Kongo

14 Machi 2022

Kiasi ya watu 30 wameuawa katika mashambulizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo kundi la waasi wa ADF linadaiwa kuhusika.

Demokratische Republik Kongo | FDLR Kämpfer
Picha: Lionel Healing/AFP/Getty Images

Habari hizo za vifo zimeripotiwa na Kinos Kathuho, mkuu wa shirika la kiraia la eneo la Mamove katika mji unaokabiliwa na machafuko wa Beni.

Amesema wapiganaji wa ADF waliingia katika kijiji cha Mambumembume Ijumaa usiku na kufanya ukatili huo akiongeza kuwa nyumba kadhaa na pikipiki zilichomwa moto na watu kadhaa hawajulikani waliko.

Makundi mengine mawili ya waasi yalikwenda katika vijiji vingine viwili jirani ambapo karibu watu watano pia waliuawa. Kathuho amesema wakaazi wanakimbilia usalama wao na hakuna kituo chochote cha jeshi katika eneo hilo.