1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 30 wauawa Nigeria

25 Januari 2024

Takribani watu 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika jimbo la katikati mwa Nigeriala la Plateau katika msururu wa mashambulizi yaliyofanywa karibu na mji wa Mangu.

Nigeria - Boko Haram
Mashambulizi ya jeshi la Nigeria dhidi ya kundi la Boko Haram mwaka 2009.Picha: picture-alliance / dpa

Hii ni licha ya kuwepo amri ya kutotembea nje usiku iliyowekwa na serikali ya jimbo hilo.

Msemaji wa kundi moja la kijamii katika eneo hilo, Joseph Gwankat, amesema washambuliaji walivilenga vijiji kadhaa, vilivyoko mpaka wa maeneo ya serikali ya mtaa ya Mangu na Barkin Ladi.

Soma zaidi: Watu 30 wauawa Nigeria

Mashambulizi ya wakulima na wafugani na migogoro ya kijamii hutokea mara kwa mara katikati mwa Nigeria, ambako mamia ya watu wameuawa katika miaka ya karibuni.

Machafuko ya Jumatano yalijiri baada ya shambulizi la Sikukuu ya Krismasi katika eneo hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu 140. Amri ya kutembea nje kuanzia jioni hadi alfajiri ilitangazwa Januari 23 mwaka huu. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW