JamiiMali
Watu 31 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Mali
28 Februari 2024Matangazo
Wizara ya uchukuzi nchini Mali imesema katika taarifa kuwa, basi hilo lilikuwa linaelekea Burkina Faso wakati ajali hiyo ilipotokea majira ya saa kumi na moja jioni.
Wizara hiyo ya uchukuzi imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva kushindwa kulidhibiti basi.
Soma pia: ECOWAS yaziondolea vikwazo Guinea, Mali
Matukio ya ajali za barabarani ni kawaida katika maeneo mengi ya Afrika Magharibi ambapo sekta ya uchukuzi wa umma imelemewa pamoja na kuwepo ukaguzi duni wa mabasi ya kubebea abiria.
Mwaka uliopita, takwimu za Umoja wa Mataifa zilionyesha kuwa bara la Afrika limeshuhudia robo ya vifo vilivyotokana na ajali za barabarani duniani licha ya bara hilo kuwa na asilimia mbili pekee ya magari kote duniani.