1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mvua kubwa yasababisha maafa Kusini Magharibi mwa China

9 Agosti 2023

Watu 33 wamethibitishwa kufa na wengine 18 bado hawajulikani waliko baada ya kushuhudiwa mvua kubwa mjini Beijing.

China | Überschwemmung in der Provinz Hebei
Picha: Yang Shiyao/ Xinhua News Agency/picture alliance

Mji huo mkuu wa China umekumbwa na kiwango kikubwa cha mvua katika wiki za karibuni, ambacho kimeharibu miundombinu na kusababisha mafuriko katika vitongoji vya jiji hilo na maeneo ya jirani.

Mafuriko katika mkoa wa kusini magharibi wa China Sichuan pia yamewauwa watu saba leo.

Watu kadhaa wamefariki katika mafuriko kaskazini mwa China, huku maafisa wa Beijing wakisema Ijumaa iliyopita kuwa vifo au kutoweka kwa watu 147 mwezi uliopita kulisababishwa na majanga ya asili.

Mamilioni ya watu wamekumbwa na matukio ya kutisha ya hali ya hewa na joto kali kote ulimwenguni. Wanasayansi wanasema matukio hayo yanazidishwa na mabadiliko ya tabianchi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW