Watu 33 wauawa kwenye shambulizi la wanamgambo Nigeria
20 Februari 2026
Matangazo
Katika taarifa aliyoitoa jana jioni, Usman amesema shambulizi hilo lilifanyika katika jamii ya Biu jimboni Kebbi.
Usman ameongeza kuwa washambuliaji hao walivuka kutoka jimbo la Sokoto, ambalo sehemu zake zinakaliwa na kundi la waasi la Lakurawa na kwamba uchunguzi wa awali unathibitisha kuwa waasi hao wenye silaha waliingia eneo hilo kuiba ng'ombe.
Hata hivyo ameongeza kuwa maafisa wa usalama wametumwa ili kurejesha na kudumisha utulivu.
Kundi la Lakurawa linafanya shughuli zake kaskazini magharibi mwa Nigeria, hasa karibu na jamii katika jimbo la Sokoto. Kundi hilo lenye silaha linajulikana kwa wizi wa mifugo, uvamizi wa vijiji na utekaji nyara ili kupata kikomboleo.