1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 35 wauawa China kufuatia ajali ya gari China

12 Novemba 2024

Watu 35 wameuawa na wengine 43 kujeruhiwa baada ya gari kuwagonga watu waliokuwa wakifanya mazoezi uwanjani katika mji wa Zhuhai ulioko kusini mwa China.

China
Watu 35 wauawa China baada ya gari kuwagonga watembea kwa miguuPicha: picture alliance/dpa/kyodo

Tukio hilo limeripotiwa jana, ingawa kwa wakati huo polisi walitoa taarifa za watu kujeruhiwa tu huku vidio za tukio hilo zikionekana kufutwa kutoka kwenye mitandao ya kijamii. 

Lakini hii leo polisi wamelitaja tukio hilo kuwa shambulio baya lililotokea katika kituo cha michezo cha Zhuhai na kutaja idadi ya watu waliopoteza maisha.

Aidha, taarifa ya polisi imesema dereva mwenye umri wa miaka 62 aliendesha gari na kulazimisha kuingia katika kituo cha michezo na kuwagonga watu waliokuwa wakifanya mazoezi ndani ya uwanja.

Rais wa China Xi Jinping ameagiza majeruhi wote wapatiwe matibabu na adhabu kwa mhusika kulingana na sheria. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW