1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Watu 4 wauwawa katika maadhimisho ya mwaka mpya Myanmar

13 Aprili 2023

Watu 4 wameuwawa mashariki mwa Myanmar leo baada ya msururu wa mabomu yaliyotegwa kwenye magari kulipuka katika sherehe za maadhimisho ya mwanzo wa mwaka mpya wa Kibuddhi.

Luftangriff auf Myanmar
Picha: Kyunhla Activists Group/AP/picture alliance

Taarifa hiyo ni kulingana na afisa mmoja wa uokoaji na duru ya usalama. Afisa huyo wa uokoaji ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa, watu 12 wamejeruhiwa na wawili wako katika hali mahututi hospitalini.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa muda mfupi kabla mchana, milipuko iliharibu karibu magari matatu mashariki mwa jimbo la Shan.

Soma pia: Utawala wa Myanmar wathibitisha kushambulia kijiji

Tangu mapinduzi yaliyofanyika Myanmar ambapo kiongozi wake Aung San Su Kyi aliondolewa madarakani, sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya za Thingyan, zimetiwa siasa ndani yake huku watetezi wa demokrasia wakitoa miita ya kususiwa kwa shughuli zilizoandaliwa na jeshi nchini humo. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW