1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 40 wauawa katika shambulizi la droni jimboni Kordofan

12 Machi 2026

Watu 40 wameuawa baada ya gari walililokuwa wamepanda wakielekea kwenye mazishi, kushambuliwa kwa droni katika eneo la Kordofan nchini Sudan.

Sudan El Obeid 2026 | Kambi ya wakimbizi wa ndani huko Kordofan Kaskazini
Kambi ya wakimbizi wa ndani huko Kordofan KaskaziniPicha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Watu 40 wameuawa baada ya gari walililokuwa wamepanda wakielekea kwenye mazishi, kushambuliwa kwa droni katika eneo la Kordofan nchini Sudan. Chanzo kimoja cha kitabibu kilichozungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa majina kwasababu za kiusalama, kimesema kwamba waliokufa wengi ni wanawake na shambulio hilo lilitokea katika barabara kati ya Abu Zabad na El-Fula, miji miwili ya jimbo la Kordofan.

Kwa karibu miaka mitatu, Sudani mekumbwa na vita kati ya jeshi la serikali na kikosi cha wanamgambo cha RSF, vita ambavyo vimeua maelfu ya watu na mamilioni kukimbia makazi.

Eneo la Kordofan, ambalo lina hazina kubwa ya mafuta na ardhi inayofaa kilimo linaunganisha ngome za RSF katika eneo la Darfur na mashariki mwa nchi inayodhibitiwa na jeshi la serikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW