1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 40,000 wayakimbia makaazi kufuatia vita Sudan magharibi

8 Januari 2020

Makabiliano yameongezeka ghafla mwishoni mwa mwezi Disemba kati ya makundi mawili pinzani na kusababisha watu kuyakimbia makaazi yao.

(Picha ya maktaba)
(Picha ya maktaba)Picha: picture-alliance/AP Photo/N. Nasser

Shirika la misaada ya kiutu la Umoja wa Mataifa, OCHA limesema makabiliano ya kikabila kati ya Waarabu na wasio waarabu katika jimbo la Darfur Magharibi nchini Sudan yamesababisha watu takriban 40,000 kuyakimbia makaazi yao, huku maelfu wakivuka mpaka na kukimbilia nchi jirani ya Chad.

Makabiliano yameongezeka ghafla mwishoni mwa mwezi Disemba kati ya makundi hayo mawili, ambapo mwarabu mmoja ameuawa kwa kuchomwa kisu. Kulingana na msemaji wa OCHA, Jens Laerke, (LEEHK)  jumla ya watu 54 wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Msemaji wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, Andrej Mahecic, (ANDREY MAHECHICH) takriban watu 3,700 ikiwa ni pamoja na wanawake 2,000 na watoto 500 wa chini ya miaka 5 wamevuka mpaka wa kati ya Darfur ya Magharibi na Chad, akisema wanaishi kwenye mazingira magumu na maeneo ya wazi, huku akitoa mwito wa misaada ya chakula na maji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW