1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu 41 wauawa katika mashambulio ya Urusi nchini Ukraine

3 Septemba 2024

Watu 41 wameauawa kutokana na mashambulio yaliyofanywa na Urusi kwenye chuo cha kijeshi katika mji wa Poltava nchini Ukraine.

Ukraine ein beschädigtes Wohnhaus
Gorofa lililoharibika kufuatia shambulio la bomu la anga la Urusi mjini Kharkiv, Ukraine. Picha: Ukrainian Emergency Service/AP/picture alliance

Watu wengine zaidi 180 walijeruhiwa katika mashambulio hayo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema shambulio hilo ni baya sana kuwahi kufanyika mnamo mwaka huu.

Zelensky ameeleza kwa njia ya video kwamba majeshi ya Urusi yalitumia makombora mawili kuharibu jengo la chuo cha mawasiliano ya kijeshi.

Soma pia: Putin asifu kasi ya vikosi vyake dhidi ya Ukraine

Wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema watu wengi wamenaswa chini ya vifusi lakini wengine zaidi ya 25 waliokolewa.

Rais wa Ukraine amesema Urusi itawajibishwa juu ya mashambulio hayo. Urusi haijasema chochote juu ya tukio hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW