1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Watu 41 wauawa katika shambulizi DRC

12 Juni 2023

Wanamgambo wenye silaha wa kundi la CODECO wameshambulia kambi ya wakimbizi katika jimbo la Ituri na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

DR Kongo Ituri UN IDP Camp
Picha: Paul Lorgerie/REUTERS

Taarifa hizo zimetolewa leo na Richard Dheda afisa tawala wa huko Bahema Badjere eneo la Djugu. Mwakilishi wa mashirika ya kiraia Desire Malodra amesema wanamgambo hao walianza kufyatua risasi na watu wengi waliteketea kwa moto katika nyumba zao huku wengine wakiuawa kwa mapanga.

Mkoa wa Ituri umekuwa ukikabiliwa na vitendo vya ghasia

Mkoa wa Ituri umekuwa ukikabiliwa na vitendo vya ghasia na mauaji. CODECO, au Ushirika kwa ajili ya Maendeleo ya Kongo, ni kundi linalodai kulinda jamii ya Lendu dhidi ya jamii ya Wahema, na pia dhidi ya jeshi la Kongo.
 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW