1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 42 wauawa katika shambulizi la waasi wa ADF Kongo

13 Juni 2024

Watu wasiopungua 42 wameuawa na waasi watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa itikadi kali katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jeshi la Uganda linawaandama waasi wa ADF mashariki mwa Kongo
Jeshi la Uganda linawaandama waasi wa ADF mashariki mwa KongoPicha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

 Msemaji wa jeshi la Kongo katika mkoa huo amethibitisha shambulizi hilo na kusema atatoa taarifa baadae. Shambulio hilo linafanana na uvamizi uliofanywa mapema wiki hii katika vijiji vya mkoa huo huo uliohusishwa na waasi hao ambao uliwauwa karibu watu 80.

Mkuu wa wilaya ya Lubero Alain Kiwewa amesema idadi ya vifo ya kati ya watu 20 na 30 imeripotiwa leo asubuhi, akiongeza kuwa idadi hiyo ni ya awali na inatarajiwa kupanda.

Amewalaumu waasi wa kundi la ADF lenye mafungamano na Dola la Kiislamu kwa kuhusika na shambulio hilo.

Afisa mwingine, kiongozi wa kijiji Macaire Sivikunula, ameliambia shirika la Reuters mapema Alhamisi kuwa watu 25 waliuawa wakiwemo wanawake sita. Pia alililaumu kundi la ADF.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW