1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 45 wauawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Mashambulizi ya kijeshi ya Israel yamewaua Wapalestina wasiopungua 45 katika Ukanda wa Gaza, wengi wao wakiwa ni katika eneo lililozingirwa la kaskazini.

Vita vya Gaza
Vita vya GazaPicha: Stringer/REUTERS

Mashambulizi ya kijeshi ya Israel yamewaua Wapalestina wasiopungua 45 katika Ukanda wa Gaza, wengi wao wakiwa ni katika eneo lililozingirwa la kaskazini, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina. Mashambulizi hayo yanafanyika mnamo wakati juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika vita vya zaidi ya mwaka mmoja, yakianza tena huko Qatar.

Watu 43 kati ya waliouawa leo Jumapili walikuwa Kaskazini mwa Gaza, ambako vikosi vya Israel vimerejea tena kuwasaka wapiganaji wa Hamas ambao inasema wamejipanga upya kwenye eneo hilo. Watu 20 waliuawa kufuatia shambulizi la kwenye nyumba katika kambi kubwa ya  wakimbizi ya Jabalia, katika Ukanda wa Gaza. Maafisa wa afya huko Gaza wanasema idadi ya watu waliouawa kutokana na kampeni ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza inakaribia kufikia alfu 43,000.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW