1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Watu 5 wameuwawa kwenye shambulio la itikadi kali Niger

16 Julai 2023

Watu watano wameuwawa na wengine kumi na tisa wamejeruhiwa katika shambulio la kigaidi kusini magharibi mwa mkoa wa Tillaberi nchini Niger.

Burkina Faso | Französische Armee
Picha: Michele Cattani/AFP/Getty Images

Taarifa ya jeshi la nchi hiyo iliyotolewa Jumamosi imesema, mauaji hayo yametokea kwenye eneo ambalo maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao wakikimbia vurugu za makundi ya itikadi kali.

Taarifa hiyo imesema shambulio hilo lilitokea Ijumaa mchana likilenga kundi la polisi waliokuwa wakisindikiza msafara katika barabara moja, karibu na eneo la mpaka wa Niger, Mali na Burkina Faso. Eneo hilo linafahamika kwa shughuli za wanamgambo wanaohusishwa na makundi ya Al-Qaeda na lile linalojiita dola la kiislamu.

Niger, moja kati ya mataifa masikini zaidi duniani, imekuwa ikipambana na machafuko yanayotokana na makundi ya itikadi kali. Machafuko hayo yamesambaa hadi kusini mashariki mwa nchi hiyo kutokea kaskazini mashariki mwa Nigeria.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW