1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 5 wauawa Mogadishu kufuatia mlipuko na mashambulizi

22 Julai 2019

Watu wasiopungua watano wameuawa mjini Mogadishu kufuatia mlipuko na mashambulizi ya risasi.

Somalia Explosion in Mogadischu
Picha: Reuters/F. Omar

Watu watano wanaripotiwa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mashambulizi kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Awali mashahidi walielezea kusikia mripuko mkubwa mapema asubuhi na kufuatiwa na milio mikubwa ya risasi.

Muuzaji wa duka moja mjini Mogadishu, Farah Hussein, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mripuko huo ulitokea katika eneo la kizuizi kwenye barabara ya K4 inayoelekea katika uwanja wa ndege wa Mogadishu.

Hadi sasa hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la Al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda mara nyingi limekuwa likifanya mashambulizi makubwa nchini Somalia.

Nchi hiyo iliyoko katika Pembe ya Afrika imekuwa ikikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 1991.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW