1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 6 wafariki kwa virusi vya Marburg nchini Rwanda

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Rwanda imethibitisha vifo vya watu 6 na visa 20 vya homa ya Marburg tangu kuanza kwa janga hilo. Waziri wa afya Sabin Nsanzimana amsema wengi wa waathirika ni wafanyakazi wa afya.

Afya | Jamii | Kirusi cha Marburg
Kirusi cha Marburg kikionekana katika darubini.Picha: Science Photo Library/IMAGO

Ugonjwa wa Marburg, ambao ni homa inayosababishwa na virusi, unaweza kusababisha kifo miongoni mwa wagonjwa, ukiwa na dalili kama vile maumivu makali ya kichwa, kutapika, maumivu ya misuli na tumbo.

Waziri Nsanzimana amesema wanafanya juhudi kutafuta watu waliotangamana na waathirika.

Homa ya Marbug ambayo ina uwezekano wa kusababisha kifo kwa asilimia 88, inatoka katika jamii moja na kirusi kinachosababisha homa ya ebola na inaambukizwa kwa watu kutoka popo wanaokula matunda, na kisha kusambaa kupitia mgusano wa kimwili na watu walioathirika.

Soma pia:Tanzania yatangaza kudhibitiwa kwa homa hatari ya Marburg

Nchi jirani ya Tanzania ilikuwa na visa vya Marburg mwaka 2023, wakati Uganda ilikuwa na visa kama hivyo mnamo mwaka wa 2017.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW