1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Watu 6 wapoteza maisha mgodini nchini Kongo

4 Machi 2026

Watu wasiopungua 6 wamekufa baada ya shimo kuporomoka kwenye mgodi wa kuchimba madini ya koltani uliopo katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Wachimbaji wadogo wa Rubaya
Maelfu ya wachimbaji wadogo wanafanya kazi katika mazingira magumu ndani ya machimbo ya koltani ya Rubaya.Picha: Zheng Yangzi/Xinhua News Agency/picture alliance

Mashahidi wameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanaume watatu na wanawake watatu wamepoteza maisha katika mgodi wa Rubaya, ulio kilometa 70 magharibi mwa mji wa Goma, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Maelfu ya wachimbaji wadogo wanafanya kazi katika mazingira magumu ndani ya machimbo ya koltani ya Rubaya yanayodhibitiwa na waasi wa M23 huku wakitumia zana duni kama chepuo na sururu. 

Mkasa huo wa maporomoko ya udongo ni wa pili kutokea katika eneo la Rubaya mnamo wiki za hivi karibu. Serikali inakadiria watu 200 walipoteza maisha katika tukio kama hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW